WhatsApp Group Join Now

NAFASI 400 za Kazi Walimu Mikoa Mbalimbali Juni 2026

Filed in Ajira by on June 3, 2026 0 Comments
NAFASI 400 za Kazi Walimu Mikoa Mbalimbali Juni 2026

NAFASI 400 za Kazi Walimu Mikoa Mbalimbali Juni 2026

Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushiriakiana na asasi ya Educate! Tanzania kupitia mradi wa kuboresha Ufundishaji na Ujifunzaji wa Somo la Elimu ya Biashara
(Business Studies), inatekeleza afua ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Biashara (Business Studies). Ofisi inatangaza nafasi 400 za walimu wa
kujitolea (mkataba) wa somo la Elimu ya Biashara kwa ajili ya shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa, kwenye mikoa ifuatayo: Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Simiyu, Kagera,
Geita, Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam. Lengo la mradi huu ni kufanikisha utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa wa Elimu ya Sekondari unaoelekeza ufundishwaji wa Somo la Elimu ya Biashara ili kuongeza ujuzi wa ujasiriamali kwa wanafunzi.

Hivyo, wahitimu wa Shahada (Degree) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kujitolea kufundisha Somo la Biashara katika shule za sekondari zitakazoorodheshwa kupitia Mfumo Rasmi wa Maombi ya ajira kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI. Muda wa kuwasilisha maombi ni kuanzia tarehe 1 Juni hadi 14 Juni, 2026. Walimu wa Kujitolea (mkataba) watakaokidhi vigezo watapangwa na kusimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

NAFASI 400 za Kazi Walimu Mikoa Mbalimbali Juni 2026

TUMA MAOMBI HAPA

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Channel Join Now!