Kikosi cha Yanga vs Azam Leo 21/06/2026

Kikosi cha Yanga vs Azam Leo 21/06/2026
Kikosi cha Yanga vs Azam Leo 21/06/2026 CRDB Federation Cup | Kikosi cha Yanga Leo dhidi ya Azam FcNusu Fainali ya CRDB Federation Cup
Leo mashabi wa Soka Tanzania wataenda kushuhudia mpambano wa aina yake kutoka kwenye Dar Derby, ikizikutanisha timu mbili mashuruli zaidi Yanga Sc vs Azamb Fc kwenye Nusu Fainali ya CRDB Federation Cup 2026 Mchezo huu unaobeba hisia za mashabiki wengi na utafanyika katika dimba la CCM Kirumba. Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa aina yake, na mashabiki wa soka wanatarajia kuona mabadiliko makubwa kwenye mbio za ubingwa huku timu hizi mbili zikiendelea kutoa burudani ya soka.
Dabi ya Dar es Salaam, mechi kati ya Azam FC na Yanga SC, ni moja ya mechi zinazoleta hamu kubwa kwa wapenzi wa soka nchini Tanzania. Timu hizi mbili zimekuwa na historia ya ushindani mkali ndani na nje ya uwanja, na kila mechi kati yao huwa na mvuto wa kipekee.
Kikosi cha Yanga Sc vs Azam Fc Leo 21/06/2026
Kikosi rasmi cha Yanga kitakacho anza leo dhidi ya Azam Fc kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 9:30 alasiri. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa na kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi.
Kikosi cha Azam Fc vs Yanga Sc Leo 21/06/2026
-Kikosi kitawekwa hapa mara baada ya kutangazwa

Djigui Diarra na Rekodi Zake Dhidi ya Azam FC
Djigui Diarra, ambaye ni kipa wa kiwango cha juu na aliyejizolea sifa kubwa kama mlinda mlango wa timu ya taifa ya Mali, ameonesha uwezo wake wa kipekee tangu alipojiunga na Yanga SC.
Hata hivyo, Diarra amekuwa akiteseka na timu ya Azam FC, ambao wamekuwa na historia ya kumfungia mabao mengi. Katika misimu minne aliyocheza na Yanga, Diarra amefungwa mabao 11 na Azam FC pekee kwenye ligi kuu ya NBC – idadi kubwa kwa mchezaji wa kiwango chake. Hii ina maana kwamba, licha ya umahiri wake, Azam FC wamekuwa na ufanisi mkubwa dhidi yake.
Pamoja na rekodi hiyo, Diarra anakaribia kufikia kiwango cha kipa maarufu wa zamani wa Tanzania, Juma Kaseja, ambaye alifungwa mabao 23 na Azam FC katika misimu tofauti akiwa na timu mbalimbali. Mashabiki wa Yanga SC wanatumai kuwa kipa wao atafanya vyema kwenye mechi hii ili kuzuia wimbi la mabao kutoka kwa washambuliaji wa Azam FC.
