WhatsApp Group Join Now

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha MOCU 24/06/2026

Filed in Usaili by on June 24, 2026 0 Comments
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha MOCU 24/06/2026

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Chuo Kikuu cha MOCU 24/06/2026

Makamu Mkuu wa Chuo,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote
walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 16/07/2026 hadi 17/07/2026 hatimaye kuwapangia
vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia
maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili
utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,
Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya
utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji anachotoka.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za nafasi husika.
5. Wasailiwa watakaowasilisha ‘Testimonials, Provisional Results, Statement of results’, hati za matokeo za kidato
cha IV na VI (‘form IV and form VI results slips’) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA
USAILI.
6. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili
pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi. Aidha kila msailiwa anapaswa kuhudhuria usaili akiwa
na mavazi nadhifu na yenye staha kulingana na Waraka wa mavazi.
8. Kwa wasailiwa waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka
husika (kama TCU, NACTVET au NECTA). Wasailiwa wa kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania
wawasilishe cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.
9. Wasailiwa ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za ‘Ajira
Portal’ na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
10. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya usaili.
Aidha wasailiwa watakaofanya usaili wa mchujo kwa njia ya Mtandao wanapaswa kukumbuka barua pepe (email
address) na nywila (password) zao wanazotumia katika mfumo wa Ajira Portal.
11. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha
Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
12. Waombaji wote wa kazi wanakumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au
kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unazingatia misingi ya haki, usawa, na uwazi, kwa kuzingatia sifa
stahiki zilizoainishwa katika tangazo la kazi husika na muundo wa utumishi wa idara inayohusika.

DOWNLOAD PDF HAPA

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WhatsApp Channel Join Now!